KCJEKCJEPamoja Tujenge Uchumi

Habari na Taarifa

Taarifa, matangazo na matukio ya hivi karibuni

KCJE KUSAMBAZA MAGUNIA MILIONI 9.3 MSIMU WA KOROSHO WA 2026/2027Makala
8 Oktoba 2026

KCJE KUSAMBAZA MAGUNIA MILIONI 9.3 MSIMU WA KOROSHO WA 2026/2027

Meneja Mkuu wa Korosho Cooperative Joint Enterprise (KCJE) Limited, Mohamed Mwinguku, amesema KCJE imejipanga kuhakikisha hakutakuwa na changamoto ya upatikanaji wa magunia katika msimu wa mauzo na masoko ya korosho wa 2026/2027. Mwinguku amesema makadirio ya uzalishaji wa korosho kwa msimu huo ni tani 750,000, huku mahitaji ya magunia yakikadiriwa kufikia zaidi ya milioni 9.35. […]

Soma zaidi
TANGAZO LA ZABUNI YA PEMBEJEO ZA KILIMOMakala
8 Oktoba 2026

TANGAZO LA ZABUNI YA PEMBEJEO ZA KILIMO

Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Cooperative Joint Enterprise Limited (KCJE Ltd), Odas Mpunga anatangaza zabuni Na. KCJE/2027/2028/G/02 kwa ajili ya ununuzi wa Pembejeo za Kilimo. Waombaji wanatakiwa kuwasilisha zabuni zao katika Ofisi za KCJE zikiwa na nakala halisi moja (1) na kivuli mbili (2) pamoja na kulipa ada isiyorejeshwa ya Sh5 milioni kupitia akaunti ya […]

Soma zaidi
RATIBA YA MINADA YA KOROSHO MSIMU WA 2026/2027Makala
8 Oktoba 2026

RATIBA YA MINADA YA KOROSHO MSIMU WA 2026/2027

Hii hapa ratiba ya minada yote ya korosho kwa msimu wa 2026/27, ikihusisha vyama wanachama sita wa KCJE, katika maeneo mbalimbali. Mnada wa kwanza utafanyika Oktoba 12, 2026 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, chini ya Chama Kikuu cha MAMCU. Baada ya hapo, minada itaendelea kwa zamu kupitia Vyama Vikuu vya TAMCU, CORECU, […]

Soma zaidi
KCJE YAONGEZA MUDA WA KUWASILISHA MAOMBI YA ZABUNI YA UJENZI WA OFISIMakala
2 Oktoba 2026

KCJE YAONGEZA MUDA WA KUWASILISHA MAOMBI YA ZABUNI YA UJENZI WA OFISI

Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Cooperative Joint Enterprise Limited (KCJE), Odas Mpunga, anautangazia umma kuwa muda wa mwisho wa kuwasilisha zabuni ya ujenzi wa ofisi ya ghorofa tano umeongezwa kwa siku saba. Zabuni hiyo yenye namba KCJE/2026/2027/W/01, iliyokuwa imepangwa kufungwa Oktoba 5, 2026, sasa itafungwa Oktoba 12, 2026 saa 5:00 asubuhi. Zabuni hiyo inalenga kumpata […]

Soma zaidi
MINADA YA KOROSHO KUANZA RASMI OKTOBA 12, 2026Makala
29 Septemba 2026

MINADA YA KOROSHO KUANZA RASMI OKTOBA 12, 2026

Minada ya msimu wa mauzo na masoko ya korosho kwa msimu wa 2026/2027 inatarajia kuanza Oktoba 12, 2026 nchini, badala ya Oktoba 19, 2026 kama ilivyotangazwa hapo awali na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT). Mabadiliko hayo yamekuja baada ya awali kutangazwa kuwa minada hiyo ingeanza Oktoba 19, huku wadau wa sekta ya korosho wakitakiwa kukamilisha […]

Soma zaidi
KCJE  YATANGAZA  ZABUNI  YA  UJENZI  WA  JENGO LA  OFISIMakala
23 Septemba 2026

KCJE YATANGAZA ZABUNI YA UJENZI WA JENGO LA OFISI

Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Cooperative Joint Enterprise Limited (KCJE Ltd), Odas Mpunga, ametangaza zabuni Na. KCJE/2026/2027/W/01 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya KCJE ya ghorofa tano katika eneo la Mtwara Mjini. Zabuni hiyo inalenga wakandarasi wenye sifa waliosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB), Daraja la I katika ujenzi wa majengo. Waombaji […]

Soma zaidi
WADAU WA KOROSHO WATAKIWA KUONGEZA UZALISHAJI, NA KUSIMAMIA UBORAMakala
28 Agosti 2026

WADAU WA KOROSHO WATAKIWA KUONGEZA UZALISHAJI, NA KUSIMAMIA UBORA

Wadau wa zao la Korosho nchini wametakiwa kuongeza kasi ya uzalishaji na kuimarisha ubora wa zao hilo ili kuiwezesha Tanzania kuwa mzalishaji namba moja wa Korosho barani Afrika. Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kigoma Malima, aliyemwakilisha Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb), wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Wadau […]

Soma zaidi
KCJE YAPOKEA TANI 5,500 ZA SALFA KUPITIA BANDARI YA MTWARAMakala
26 Agosti 2026

KCJE YAPOKEA TANI 5,500 ZA SALFA KUPITIA BANDARI YA MTWARA

Kaimu Meneja Mkuu wa Korosho Cooperative Joint Enterprise (KCJE) Limited, Spicener Rugalela, amesema taasisi hiyo imepokea shehena ya tani 5,500 za salfa ya unga katika Bandari ya Mtwara kwa ajili ya kuendelea kusambaza kwa wakulima wa korosho katika msimu wa 2026/2027. Rugalela amesema KCJE imelenga kusambaza jumla ya tani 35,000 za salfa kwa wakulima katika […]

Soma zaidi
TANCCOOPS YAITEMBELEA  KCJE, KUJIFUNZA UZOEFU WA KUHUDUMIA WAKULIMAMakala
18 Agosti 2026

TANCCOOPS YAITEMBELEA KCJE, KUJIFUNZA UZOEFU WA KUHUDUMIA WAKULIMA

Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vinavyolima zao la Pamba nchini (TANCCOOPS), ulifanya ziara mkoani Mtwara kwa lengo la kuitembelea Korosho Cooperative Joint Enterprise (KCJE) Limited ili kujifunza kuhusu shughuli, mifumo na uzoefu wa taasisi hiyo katika kuendeleza sekta ya kilimo. Ziara hiyo ya siku tatu ilianza Agosti 18, 2026 mkoani Mtwara, ikiwa […]

Soma zaidi
NAIBU WAZIRI WA KILIMO ATEMBELEA BANDA LA KCJE NGONGO LINDIMakala
6 Agosti 2026

NAIBU WAZIRI WA KILIMO ATEMBELEA BANDA LA KCJE NGONGO LINDI

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde, alitembelea banda la Korosho Cooperative Joint Enterprise (KCJE) Limited katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini yaliyofanyika katika Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi. Ziara hiyo ililenga kujionea huduma na teknolojia mbalimbali zinazotolewa na KCJE katika kuimarisha sekta ya Korosho na maendeleo ya Ushirika nchini. Akiwa katika banda hilo, […]

Soma zaidi
MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MTWARA KCJE IMELETA MABADILIKO MAKUBWA KATIKA SEKTA YA KOROSHOMakala
15 Julai 2026

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MTWARA KCJE IMELETA MABADILIKO MAKUBWA KATIKA SEKTA YA KOROSHO

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara, Mwl. Saidi Nyengedi, ameipongeza Korosho Cooperative Joint Enterprise (KCJE) Limited kwa mafanikio makubwa iliyoyapata katika kipindi cha miaka minne tangu kuanzishwa kwake, akisema taasisi hiyo imekuwa mfano wa utekelezaji wa dhana ya ushirika katika kukuza uchumi wa wakulima wa korosho nchini. Mwl. Nyengedi alitoa pongezi hizo […]

Soma zaidi
MWAIPAYA AIPONGEZA KCJE KWA MAFANIKIO MAKUBWA SEKTA YA KOROSHOMakala
15 Julai 2026

MWAIPAYA AIPONGEZA KCJE KWA MAFANIKIO MAKUBWA SEKTA YA KOROSHO

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Abdallah Mwaipaya, ameipongeza Korosho Cooperative Joint Enterprise (KCJE) Limited kwa mafanikio makubwa iliyoyapata katika kuimarisha sekta ya korosho nchini, akisema taasisi hiyo imekuwa nguzo muhimu ya kuinua uchumi wa wakulima na kuimarisha Ushirika. Akizungumza wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa Tano wa KCJE Limited, uliofanyika Julai 15, 2026 mkoani Mtwara, […]

Soma zaidi
VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA WATAKIWA KUZINGATIA UTAWALA BORAMakala
14 Julai 2026

VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA WATAKIWA KUZINGATIA UTAWALA BORA

Viongozi wa Vyama vya Ushirika nchini wametakiwa kuzingatia misingi ya uongozi na utawala bora ili kuongeza uwajibikaji, uwazi na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wanachama, hatua inayotazamiwa kuchochea maendeleo ya vyama hivyo na kuongeza tija kwa wakulima. Wito huo umetolewa na Mhadhiri na Mratibu wa Programu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) ofisi […]

Soma zaidi
KCJE YAJIVUNIA MAFANIKIO YA KUONGEZA UZALISHAJI WA KOROSHO, YAWEKA MIKAKATI YA UWEKEZAJIMakala
14 Julai 2026

KCJE YAJIVUNIA MAFANIKIO YA KUONGEZA UZALISHAJI WA KOROSHO, YAWEKA MIKAKATI YA UWEKEZAJI

Ushirikiano wa Vyama Vikuu vya Ushirika vinavyounda Korosho Cooperative Joint Enterprise (KCJE) Limited umeendelea kuimarisha sekta ya korosho nchini, huku hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika usambazaji wa pembejeo zikichangia kuongezeka kwa uzalishaji wa zao hilo na kuboresha huduma kwa wakulima. Hayo yameelezwa na Meneja Mkuu wa KCJE, Mohamed Mwinguku, wakati akiwasilisha mada kuhusu shughuli, mafanikio, changamoto […]

Soma zaidi
KCJE YAWAJENGEA UWEZO WADAU, YASIFIWA KWA KUIMARISHA USHIRIKA NA TIJA KWA WAKULIMAMakala
14 Julai 2026

KCJE YAWAJENGEA UWEZO WADAU, YASIFIWA KWA KUIMARISHA USHIRIKA NA TIJA KWA WAKULIMA

Korosho Cooperative Joint Enterprise (KCJE) Limited imeendelea kupongezwa kwa juhudi zake za kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya Ushirika, kupitia mafunzo yanayolenga kuongeza uelewa kuhusu shughuli, majukumu na huduma zinazotolewa na taasisi hiyo. Pongezi hizo zimetolewa na Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Mtwara, Robert Nsunza, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wadau […]

Soma zaidi
NDEGE NYUKI (DRONE)Makala
21 Aprili 2026

NDEGE NYUKI (DRONE)

Leo katika ofisi za KCJE Ltd, tumepokea wageni kutoka MAT Technology wakiambatana na TCDC kwa ajili ya kuwasilisha teknolojia ya kisasa ya matumizi ya drone (ndege nyuki) katika kilimo cha korosho.KCJE Ltd imeshiriki kikao, kilichofanyika katika ukumbi wa Tiffany Diamond Hotel, Mtwara. Katika kikao hicho, wataalamu kutoka MAT Technology waliwasilisha matumizi ya teknolojia ya drone […]

Soma zaidi
SALAMU ZA HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYAHabari
24 Desemba 2025

SALAMU ZA HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYA

Uongozi wa Korosho Cooperative Joint Enterprise Ltd (KCJE Ltd) unapenda kutoa salamu za Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya kwa wanachama wote, wadau, washirika wa maendeleo, na watu wote kwa ujumla. Tunatoa shukrani za dhati kwa ushirikiano, uaminifu na mchango wenu katika kuendeleza sekta ya korosho na kuimarisha shughuli za ushirika kwa mwaka mzima uliopita. […]

Soma zaidi
UTOAJI WA VYETI KWA VYAMA WANACHAMA WA KCJE LTDMakala
18 Desemba 2025

UTOAJI WA VYETI KWA VYAMA WANACHAMA WA KCJE LTD

Katika hatua nyingine muhimu, kikao cha Ushirika wa Mradi wa Pamoja wa Korosho (KCJE Ltd) pia kiliambatana na zoezi la ugawaji wa vyeti kwa Vyama Wanachama vilivyokidhi masharti ya uanachama kwa mujibu wa katiba na miongozo ya ushirika. Vyeti hivyo vilitolewa kwa vyama vilivyofanikiwa kulipa ada ya kiingilio pamoja na kukamilisha ununuzi wa hisa zote, […]

Soma zaidi
ROTAI YAKABIDHI ZAWADI ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA KWA KCJE LTDMakala
15 Desemba 2025

ROTAI YAKABIDHI ZAWADI ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA KWA KCJE LTD

Katika kuadhimisha msimu wa sikukuu, kampuni ya ROTAI—ambayo ni miongoni mwa wazabuni wakubwa na wa kuaminika wa mizani za kidigitali nchini—imekabidhi zawadi maalumu za Krismasi na Mwaka Mpya (Merry Christmas and Happy New Year) kwa KCJE Ltd. Zawadi hizi zimewasilishwa kama ishara ya kuthamini ushirikiano mzuri na wa muda mrefu uliopo kati ya ROTAI na […]

Soma zaidi
KCJE LTD YAPOKEA UGENI WA MAAFISA WA KILIMO KUTOKA WIZARA YA KILIMOHabari
2 Desemba 2025

KCJE LTD YAPOKEA UGENI WA MAAFISA WA KILIMO KUTOKA WIZARA YA KILIMO

Maafisa wa Ushirika kutoka Wizara ya Kilimo wametembelea Ushirika wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Korosho (KCJE Ltd) kwa lengo la kuangazia na kukagua mnyororo wa upokeaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo, viuatilifu pamoja na magunia kwa wakulima wa korosho. Katika ziara hiyo, maafisa hao walipata fursa ya kujionea kwa karibu mfumo […]

Soma zaidi
CRDB Bank Yatembelea KCJE LtdHabari
21 Novemba 2025

CRDB Bank Yatembelea KCJE Ltd

Tarehe 20/11/2025, KCJE Ltd tumepokea ugeni kutoka CRDB Bank katika ziara maalum ya kuona shehena za viuatilifu na magunia yaliyowasilishwa na kampuni ambazo zimepatiwa mikopo na benki hiyo. Ziara hiyo ilihusisha ukaguzi wa shehena kutoka kwa wazabuni wanaoshirikiana na KCJE Ltd katika kusambaza pembejeo muhimu zinazowawezesha wakulima kuongeza uzalishaji—hususan kwenye zao la korosho. Akizungumza kwa […]

Soma zaidi
Ziara ya Viongozi wa KCJE Maghalani kuelekea Msimu wa KoroshoMakala
19 Septemba 2025

Ziara ya Viongozi wa KCJE Maghalani kuelekea Msimu wa Korosho

Katika kipindi hiki cha maandalizi kuelekea msimu wa korosho, Mwenyekiti wa Bodi ya Wajumbe wa Korosho Cooperative Joint Enterprise Ltd (KCJE), Ndugu Odas Odas, akiwa ameambatana na Afisa Masoko wa KCJE, Ndugu Methew Rajab, wamefanya ziara maalum katika maghala ya kuhifadhia vifungashio na viuatilifu yaliyopo Wilaya ya Masasi, Mkoa wa Mtwara. 🔍 Lengo la ziara […]

Soma zaidi
Maonesho ya Nane Nane Ngongo mkoani Lindi 2025Makala
8 Agosti 2025

Maonesho ya Nane Nane Ngongo mkoani Lindi 2025

Maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika Ngongo Mkoani Lindi mwaka 2025 kanda ya Kusini Tanzania. KCJE Ltd Ilionesha bidhaa zake na Wageni mbali mbali walifika na kutembelea Banda la KCJE katika maeneo ya Ushirika (Kijiji cha Ushirika). Moja ya Wageni waliotembelea ni Pamoja na Mh. Victoria Mwanziva DC Lindi.

Soma zaidi