KCJEKCJEPamoja Tujenge Uchumi
Habari na Taarifa
Habari

KCJE LTD YAPOKEA UGENI WA MAAFISA WA KILIMO KUTOKA WIZARA YA KILIMO

2 Desemba 2025KCJE
KCJE LTD YAPOKEA UGENI WA MAAFISA WA KILIMO KUTOKA WIZARA YA KILIMO

Maafisa wa Ushirika kutoka Wizara ya Kilimo wametembelea Ushirika wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Korosho (KCJE Ltd) kwa lengo la kuangazia na kukagua mnyororo wa upokeaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo, viuatilifu pamoja na magunia kwa wakulima wa korosho.

Katika ziara hiyo, maafisa hao walipata fursa ya kujionea kwa karibu mfumo unaotumiwa na KCJE Ltd katika kupokea, kuhifadhi na kusambaza pembejeo na vifaa muhimu kwa wakulima kupitia vyama vikuu vya ushirika. Lengo kuu likiwa ni kuhakikisha huduma hizo zinafika kwa wakati, kwa uwazi na kwa ubora unaokidhi viwango vinavyotakiwa.

Ziara hiyo pia ilihusisha majadiliano kuhusu changamoto zinazojitokeza katika mnyororo wa usambazaji wa pembejeo pamoja na mikakati ya pamoja ya kuboresha huduma hizo ili kuongeza tija katika uzalishaji wa korosho.


Mradi wa Ushirika wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya korosho (KCJE Ltd) unaendelea kudhihirisha mchango wake mkubwa katika kuimarisha ushirika, uchumi wa wakulima, na maendeleo ya Taifa.

Habari Zinazohusiana

SALAMU ZA HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYAHabari
24 Desemba 2025

SALAMU ZA HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYA

Uongozi wa Korosho Cooperative Joint Enterprise Ltd (KCJE Ltd) unapenda kutoa salamu za Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya kwa wanachama wote, wadau, washirika wa maendeleo, na watu wote kwa ujumla. Tunatoa shukrani za dhati kwa ushirikiano, uaminifu na mchango wenu katika kuendeleza sekta ya korosho na kuimarisha shughuli za ushirika kwa mwaka mzima uliopita. […]

Soma zaidi
CRDB Bank Yatembelea KCJE LtdHabari
21 Novemba 2025

CRDB Bank Yatembelea KCJE Ltd

Tarehe 20/11/2025, KCJE Ltd tumepokea ugeni kutoka CRDB Bank katika ziara maalum ya kuona shehena za viuatilifu na magunia yaliyowasilishwa na kampuni ambazo zimepatiwa mikopo na benki hiyo. Ziara hiyo ilihusisha ukaguzi wa shehena kutoka kwa wazabuni wanaoshirikiana na KCJE Ltd katika kusambaza pembejeo muhimu zinazowawezesha wakulima kuongeza uzalishaji—hususan kwenye zao la korosho. Akizungumza kwa […]

Soma zaidi