KCJEKCJEPamoja Tujenge Uchumi
新闻动态
Makala

Ziara ya Viongozi wa KCJE Maghalani kuelekea Msimu wa Korosho

2025年9月19日KCJE
Ziara ya Viongozi wa KCJE Maghalani kuelekea Msimu wa Korosho

Katika kipindi hiki cha maandalizi kuelekea msimu wa korosho, Mwenyekiti wa Bodi ya Wajumbe wa Korosho Cooperative Joint Enterprise Ltd (KCJE), Ndugu Odas Odas, akiwa ameambatana na Afisa Masoko wa KCJE, Ndugu Methew Rajab, wamefanya ziara maalum katika maghala ya kuhifadhia vifungashio na viuatilifu yaliyopo Wilaya ya Masasi, Mkoa wa Mtwara. 🔍

Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kufuatilia kwa karibu hali ya upatikanaji pamoja na viwango vya vifungashio na viuatilifu vilivyopo kwa sasa, ili kuhakikisha maandalizi ya msimu wa korosho yanafanyika kwa ufanisi na kwa wakati.

KCJE inaendelea kujizatiti kuhakikisha wakulima wanapata huduma bora na vifaa vinavyokidhi viwango, kwa lengo la kuimarisha mnyororo wa thamani wa zao la korosho nchini.

相关文章

KCJE KUSAMBAZA MAGUNIA MILIONI 9.3 MSIMU WA KOROSHO WA 2026/2027Makala
2026年10月8日

KCJE KUSAMBAZA MAGUNIA MILIONI 9.3 MSIMU WA KOROSHO WA 2026/2027

Meneja Mkuu wa Korosho Cooperative Joint Enterprise (KCJE) Limited, Mohamed Mwinguku, amesema KCJE imejipanga kuhakikisha hakutakuwa na changamoto ya upatikanaji wa magunia katika msimu wa mauzo na masoko ya korosho wa 2026/2027. Mwinguku amesema makadirio ya uzalishaji wa korosho kwa msimu huo ni tani 750,000, huku mahitaji ya magunia yakikadiriwa kufikia zaidi ya milioni 9.35. […]

阅读更多
TANGAZO LA ZABUNI YA PEMBEJEO ZA KILIMOMakala
2026年10月8日

TANGAZO LA ZABUNI YA PEMBEJEO ZA KILIMO

Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Cooperative Joint Enterprise Limited (KCJE Ltd), Odas Mpunga anatangaza zabuni Na. KCJE/2027/2028/G/02 kwa ajili ya ununuzi wa Pembejeo za Kilimo. Waombaji wanatakiwa kuwasilisha zabuni zao katika Ofisi za KCJE zikiwa na nakala halisi moja (1) na kivuli mbili (2) pamoja na kulipa ada isiyorejeshwa ya Sh5 milioni kupitia akaunti ya […]

阅读更多