
KOROSHO TANI 49,093 ZENYE THAMANI YA ZAIDI BILIONI 160 ZAUZWA WIKI YA KWANZA YA MINADA

Jumla ya kilo 49,093,143 sawa na tani 49,093.143 za korosho ghafi zenye thamani ya shilingi bilioni 160 zimeuzwa katika minada minne iliyoendeshwa na Vyama Vikuu vya Ushirika vya mikoa ya Lindi na Mtwara, katika wiki ya kwanza ya msimu wa mauzo ya korosho wa mwaka 2026/2027.
Minada hiyo ilianza Oktoba 12 na 13, 2026, kupitia Chama Kikuu cha Ushirika MAMCU, kilichouza jumla ya kilo 11,585,342 sawa na tani 11,585.342, kwa bei ya juu ya Sh3,370 na ya chini ya Sh3,110 kwa kilo.
Oktoba 16, 2026, Chama Kikuu cha Ushirika TANECU kiliendesha mnada wake wa kwanza na kuuza kilo 18,991,115 sawa na tani 18,991.115, kwa bei ya juu ya Sh3,430 na ya chini ya Sh3,250 kwa kilo.
Oktoba 17, 2026, Chama Kikuu cha Ushirika Lindi Mwambao Ltd kiliendesha mnada wake wa kwanza katika AMCOS ya Mtama, na kuuza kilo 7,685,914 sawa na tani 7,685.914, kwa bei ya juu ya Sh3,280 na ya chini ya Sh2,970 kwa kilo.
Oktoba 18, 2026, Chama Kikuu cha Ushirika RUNALI kiliendesha mnada wake wa kwanza na kufanikiwa kuuza kilo 10,830,772 sawa na tani 10,830.772 za korosho ghafi, kwa bei ya juu ya Sh3,430 na bei ya chini Sh3,270.
Akizungumzia mwenendo wa minada hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Francis Alfred, amesema mauzo hayo yanaonesha ukubwa wa biashara ya korosho na umuhimu wa kusimamia kikamilifu mfumo wa masoko ili kuhakikisha zao hilo linapata thamani inayostahili.
Alfred amewasisitiza wakulima kuzingatia ubora wa korosho kuanzia hatua za uvunaji, ukaushaji, ukusanyaji hadi uhifadhi ili kuongeza ubora na ushindani wa zao hilo sokoni.
Minada yote inaendeshwa kidijitali kupitia mfumo wa soko la bidhaa hapa nchini (TMX).
Artigos relacionados
MakalaKCJE KUSAMBAZA MAGUNIA MILIONI 9.3 MSIMU WA KOROSHO WA 2026/2027
Meneja Mkuu wa Korosho Cooperative Joint Enterprise (KCJE) Limited, Mohamed Mwinguku, amesema KCJE imejipanga kuhakikisha hakutakuwa na changamoto ya upatikanaji wa magunia katika msimu wa mauzo na masoko ya korosho wa 2026/2027. Mwinguku amesema makadirio ya uzalishaji wa korosho kwa msimu huo ni tani 750,000, huku mahitaji ya magunia yakikadiriwa kufikia zaidi ya milioni 9.35. […]
Ler mais
MakalaTANGAZO LA ZABUNI YA PEMBEJEO ZA KILIMO
Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Cooperative Joint Enterprise Limited (KCJE Ltd), Odas Mpunga anatangaza zabuni Na. KCJE/2027/2028/G/02 kwa ajili ya ununuzi wa Pembejeo za Kilimo. Waombaji wanatakiwa kuwasilisha zabuni zao katika Ofisi za KCJE zikiwa na nakala halisi moja (1) na kivuli mbili (2) pamoja na kulipa ada isiyorejeshwa ya Sh5 milioni kupitia akaunti ya […]
Ler mais
MakalaRATIBA YA MINADA YA KOROSHO MSIMU WA 2026/2027
Hii hapa ratiba ya minada yote ya korosho kwa msimu wa 2026/27, ikihusisha vyama wanachama sita wa KCJE, katika maeneo mbalimbali. Mnada wa kwanza utafanyika Oktoba 12, 2026 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, chini ya Chama Kikuu cha MAMCU. Baada ya hapo, minada itaendelea kwa zamu kupitia Vyama Vikuu vya TAMCU, CORECU, […]
Ler mais