KCJEKCJEPamoja Tujenge Uchumi
Notizie e aggiornamenti
Habari

CRDB Bank Yatembelea KCJE Ltd

21 novembre 2025KCJE
CRDB Bank Yatembelea KCJE Ltd

Tarehe 20/11/2025, KCJE Ltd tumepokea ugeni kutoka CRDB Bank katika ziara maalum ya kuona shehena za viuatilifu na magunia yaliyowasilishwa na kampuni ambazo zimepatiwa mikopo na benki hiyo.

Ziara hiyo ilihusisha ukaguzi wa shehena kutoka kwa wazabuni wanaoshirikiana na KCJE Ltd katika kusambaza pembejeo muhimu zinazowawezesha wakulima kuongeza uzalishaji—hususan kwenye zao la korosho.

Akizungumza kwa niaba ya KCJE Ltd, Kaimu Afisa Masoko Bw. Mathew Rajabu, aliishukuru CRDB kwa kuendelea kutoa mikopo inayowawezesha wazabuni kuleta bidhaa kwa wakati. Ushirikiano huu unaimarisha mnyororo wa thamani na kuchochea maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.

Articoli correlati

SALAMU ZA HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYAHabari
24 dicembre 2025

SALAMU ZA HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYA

Uongozi wa Korosho Cooperative Joint Enterprise Ltd (KCJE Ltd) unapenda kutoa salamu za Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya kwa wanachama wote, wadau, washirika wa maendeleo, na watu wote kwa ujumla. Tunatoa shukrani za dhati kwa ushirikiano, uaminifu na mchango wenu katika kuendeleza sekta ya korosho na kuimarisha shughuli za ushirika kwa mwaka mzima uliopita. […]

Leggi di più
KCJE LTD YAPOKEA UGENI WA MAAFISA WA KILIMO KUTOKA WIZARA YA KILIMOHabari
2 dicembre 2025

KCJE LTD YAPOKEA UGENI WA MAAFISA WA KILIMO KUTOKA WIZARA YA KILIMO

Maafisa wa Ushirika kutoka Wizara ya Kilimo wametembelea Ushirika wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Korosho (KCJE Ltd) kwa lengo la kuangazia na kukagua mnyororo wa upokeaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo, viuatilifu pamoja na magunia kwa wakulima wa korosho. Katika ziara hiyo, maafisa hao walipata fursa ya kujionea kwa karibu mfumo […]

Leggi di più