KCJEKCJEPamoja Tujenge Uchumi
Actualités
Makala

KCJE LTD YAENDELEA NA MAANDALIZI YA PEMBEJEO NA VIUATILIFU KWA MSIMU WA KOROSHO 2026/2027

6 mars 2026KCJE
KCJE LTD YAENDELEA NA MAANDALIZI YA PEMBEJEO NA VIUATILIFU KWA MSIMU WA KOROSHO 2026/2027

Ushirika wa Mradi wa Pamoja wa Korosho (KCJE Ltd) una jukumu muhimu la kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo na viuatilifu bora kwa ajili ya uzalishaji wa korosho kwa wakati muafaka.

Katika kujiandaa na msimu mpya wa korosho wa mwaka 2026/2027, ushirika unaendelea na maandalizi mbalimbali ya kuhakikisha pembejeo pamoja na viuatilifu vinapatikana kwa wingi na kwa wakati ili kuwasaidia wakulima kuongeza tija na ubora wa mazao yao.

Hatua hizi ni sehemu ya juhudi za KCJE Ltd katika kuimarisha uzalishaji wa korosho, kuongeza kipato cha wakulima, na kuchangia maendeleo ya sekta ya korosho nchini. Ushirika utaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha wakulima wanapata huduma bora zinazowezesha uzalishaji wenye tija na endelevu.

Articles liés

KCJE KUSAMBAZA MAGUNIA MILIONI 9.3 MSIMU WA KOROSHO WA 2026/2027Makala
8 octobre 2026

KCJE KUSAMBAZA MAGUNIA MILIONI 9.3 MSIMU WA KOROSHO WA 2026/2027

Meneja Mkuu wa Korosho Cooperative Joint Enterprise (KCJE) Limited, Mohamed Mwinguku, amesema KCJE imejipanga kuhakikisha hakutakuwa na changamoto ya upatikanaji wa magunia katika msimu wa mauzo na masoko ya korosho wa 2026/2027. Mwinguku amesema makadirio ya uzalishaji wa korosho kwa msimu huo ni tani 750,000, huku mahitaji ya magunia yakikadiriwa kufikia zaidi ya milioni 9.35. […]

Lire la suite
TANGAZO LA ZABUNI YA PEMBEJEO ZA KILIMOMakala
8 octobre 2026

TANGAZO LA ZABUNI YA PEMBEJEO ZA KILIMO

Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Cooperative Joint Enterprise Limited (KCJE Ltd), Odas Mpunga anatangaza zabuni Na. KCJE/2027/2028/G/02 kwa ajili ya ununuzi wa Pembejeo za Kilimo. Waombaji wanatakiwa kuwasilisha zabuni zao katika Ofisi za KCJE zikiwa na nakala halisi moja (1) na kivuli mbili (2) pamoja na kulipa ada isiyorejeshwa ya Sh5 milioni kupitia akaunti ya […]

Lire la suite