KCJEKCJEPamoja Tujenge Uchumi
الأخبار والمستجدات
Makala

Mkutano Mkuu wa Nne wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika wa Korosho (KCJE) Wafanyika Kwa Mafanikio

25 يوليو 2025KCJE
Mkutano Mkuu wa Nne wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika wa Korosho (KCJE) Wafanyika Kwa Mafanikio

Tarehe 21 Julai 2025, Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika wa Korosho (KCJE) umefanya Mkutano Mkuu wa Nne (4) katika ukumbi wa Shangani Beach Hotel, Mjini Mtwara.

Mkutano huo umehusisha viongozi wa vyama vikuu vya ushirika ambao, Warajis Wasaidizi, Wazabuni wa Pembejeo na Magunia, wadau wa sekta ya korosho, Mbaazi na Ufuta pamoja na washirika mbalimbali.

Ajenda kuu, malengo ya kikao, maazimio au mambo yaliyojadiliwa:

Mkutano huo uliangazia tathmini ya utekelezaji wa shughuli za mradi kwa mwaka uliopita,

kupanga mikakati ya mwaka ujao, na kuimarisha ushirikiano kati ya vyama vikuu.

Viongozi walisisitiza umuhimu wa uwazi, ushirikiano wa karibu na matumizi sahihi ya rasilimali ili kuinua kilimo cha korosho nchini.

Hotuba na Washiriki Wakuu

Mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa NANJIVA NZUNDA Ras Msaidizi wa Uchumi na Udhalishaji, ambaye alisisitiza dhamira ya serikali katika kuimarisha sekta ya ushirika. Wengine walioshiriki ni pamoja na Odas O. Mpunga, Mwenyekiti wa Bodi ya KCJE, na wawakilishi kutoka CBT, TPHPA na WMA.

Mradi wa KCJE unaendelea kuwa mfano bora wa ushirikiano miongoni mwa vyama vya ushirika nchini, na kupitia mikutano kama hii, wadau wote wanapata nafasi ya kujifunza, kushirikiana na kuweka mikakati madhubuti kwa maendeleo ya sekta ya korosho na Ushirika Tanzania.

مقالات ذات صلة

KCJE KUSAMBAZA MAGUNIA MILIONI 9.3 MSIMU WA KOROSHO WA 2026/2027Makala
8 أكتوبر 2026

KCJE KUSAMBAZA MAGUNIA MILIONI 9.3 MSIMU WA KOROSHO WA 2026/2027

Meneja Mkuu wa Korosho Cooperative Joint Enterprise (KCJE) Limited, Mohamed Mwinguku, amesema KCJE imejipanga kuhakikisha hakutakuwa na changamoto ya upatikanaji wa magunia katika msimu wa mauzo na masoko ya korosho wa 2026/2027. Mwinguku amesema makadirio ya uzalishaji wa korosho kwa msimu huo ni tani 750,000, huku mahitaji ya magunia yakikadiriwa kufikia zaidi ya milioni 9.35. […]

اقرأ المزيد
TANGAZO LA ZABUNI YA PEMBEJEO ZA KILIMOMakala
8 أكتوبر 2026

TANGAZO LA ZABUNI YA PEMBEJEO ZA KILIMO

Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Cooperative Joint Enterprise Limited (KCJE Ltd), Odas Mpunga anatangaza zabuni Na. KCJE/2027/2028/G/02 kwa ajili ya ununuzi wa Pembejeo za Kilimo. Waombaji wanatakiwa kuwasilisha zabuni zao katika Ofisi za KCJE zikiwa na nakala halisi moja (1) na kivuli mbili (2) pamoja na kulipa ada isiyorejeshwa ya Sh5 milioni kupitia akaunti ya […]

اقرأ المزيد